• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
Sikonge District Council
Sikonge District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Idadi ya Watu
      • Hali ya Hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Mifugo na uvuvi
      • Afya na Ustawi wa jamii
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mazingira na Taka ngumu
      • Kilimo, Umwagilaji na Ushirika
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Uchimbaji wa Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo Ndogo
    • Miongozo Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya sanaa
      • Sanaa za picha
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba
    • Habari mpya
    • Matukio

KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIKONGE AONGOZA MENEJIMENTI KUKAGUA MIRADI INAYOPENDEKEZWA KUFIKIWA NA MWENGE WA UHURU 2024.

Imewekwa: April 19th, 2024

Kaimu Mkurugenzi Mtedaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bw. Bwenge Mwesigwa ameongoza timu ya menejimenti kukagua miradi inayopendekezwa kufikiwa na mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu 2024.

Kati ya miradi iliyokaguliwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa kisima kirefu cha pampu ya umeme chenye urefu wa mita 101 katika shule ya msingi Muungano iliyopo kata ya Mole.Mradi huu una gharama ya kiasi cha shilingi milioni 45 , kisima hiki kikikamilika kina uwezo wa kutoa lita za maji 14,500 kwa saa.Mradi umefika asilimia 60% na tayari mkandarasi wa mradi huu yupo katika hatua za mwisho za kuanza kazi ya umaliziaji wa kisima hicho.

Mradi mwingine uliokaguliwa na menejimenti ni ujenzi wa kituo cha afya Igigwa  kilichopo kata ya igigwa chenye thamani ya shilingi milioni 332.8.Mradi huu unahusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD),maabara,shimo la kutupia  kondo la nyuma ,vyoo vya nje pamoja na kichomea taka,mradi wa ujenzi umefikia asilimia 95%.

Vilevile menejimenti imezuru shule ya sekondari Kamagi kukagua mradi wa ujenzi wakuongeza miundombinu ya kidato cha tano na sita,uliopo kata ya Misheni,mradi huo unahusisha ujenzi wa vyumba 9 vya madarasa,mabweni  4 pamoja na ujenzi wa matundu 14 ya vyoo.Mradi unagharimu shilingi milioni 808 na mradi umekamilika.

Mradi wa mwisho uliotembelewa na  menejimenti ni mradi wa vijana wa ushonaji  wa nguo,uliopo eneo Sikonge madukani,kata ya Sikonge,mradi unagharama ya shilingi  milioni 16 ikiwa ni  mkopo wa kuwakwamua  vijana kiuchumi toka halmashauri unaohusisha vijana 05,mradi unaendelea vizuri.

Akijumuisha ukaguzi huo Kaimu mkurugenzi ameagiza ukamilishwaji wa miradi kwa haraka hususani mradi wa kisima kirefu cha maji katika shule ya msingi Muungano  na kusafisha maeneo yote yanayozunguka eneo la ujenzi wa kituo cha afya Igigwa.

Aidha amemuagiza mweyekiti wa kikundi cha vijana cha  ushonaji wa nguo kuwasilisha taarifa ya marejesho ya kikundi hicho pamoja na stakabadhi za malighafi zote walizonunua kiwandani hapo.

Ziara hii ni maandalizi ya mbio za mwenge wa uhuru 2024 ambazo zilizinduliwa rasmi Aprili 2, 2024 mkoani Kilimanjaro na zinatarajiwa kufika mkoani Tabora Agosti 16, 2024,zikiongozwa na kauli mbiu isemayo “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”.




Matangazo

  • TANGAZO LA ZABUNI YA KUKODISHA CANTEEN [MGAHAWA] MPYA KWENYE JENGO LA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZAABUNI YA KUMPATA MWEKEZAJI KATIKA KIWANDA CHA KATI CHA KUCHAKATA MAZAO YA NYUKI(MARUDIO) June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA USAFI KWENYE OFISI ZA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA ULINZI June 07, 2023
  • Angalia zaidi

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA UMMA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIKONGE WAPIGWA MSASA JUU YA MATUMIZI YA MFUMO WA E-UTENDAJI (PEPMIS)

    June 25, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA SIKONGE YAPATA HATI INAYORIDHISHA TAARIFA YA UKAGUZI YA MWAKA 2023/2024

    June 14, 2025
  • UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA WAPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO KUTOKA 74% HADI 43% WILAYANI SIKONGE

    June 13, 2025
  • VIJIJI 16 KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIKONGE KUNUFAIKA NA PROGRAMU YA UANDAAJI WA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI

    June 06, 2025
  • Angalia zaidi

Video

Ziara ya Waheshimiwa Madiwani Wilayani Rungwe - Mbeya.
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Matangazo
  • Zabuni
  • Matukio
  • Habari

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Mkoa wa Tabora
  • TAMISEMI
  • Urambo DC
  • UTUMISHI
  • Kaliua DC

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC

    Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora

    Simu: 0767135460

    Simu: 0767135460

    Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma zetu

Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa