Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bw. Nico Kayange amewaongoza Wakuu wa Idara na Divisheni katika ukaguzi wa ujenzi wa mnada wa Mifugo wa Mlogolo ambapo ujenzi wa uzio wa mnada umekamilika.
Bw. Kayange ameagiza ujenzi uliobaki wa miundombinu ya msingi ambayo ni Choo cha Mnada vikamilike ndani ya Mwezi mmoja ili mnada uanze kufanya kazi.
Mradi wa ujenzi wa uzio wa mnada umegharimu Shilingi 227,826,140. Tayari Shilingi 17,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa choo zimeshatolewa.
Kwa upande wa ukarabati wa Machinjio ya Wilaya bado unaendelea kwa awamu ya pili,ambapo kiasi cha shilingi 5,000,000/= zilishatumika kwa awamu ya kwanza kwa ajili ya ukarabati wa sakafu ya machinjio na kuezeka banda la kuanikia Ngozi.
Aidha shilingi 15,000,000/= zilishatolewa kwa ajili ya ukarabati awamu ya pili ikihusisha gharama za kuleta nguzo za umeme toka Kambi ya Wahandisi TANROADS kuja machinjioni,Kununua vifaa vya umeme,kufanya uhandisi wa umeme na kujenga mfereji wa nje wa maji taka, kazi inaendelea kwa kiwango cha kuridhisha.
Kwa upande wa ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Sikonge akitoa maelezo ya jumla Kaimu Mkurugenzi ameshauri kasi ya ujenzi iongezeke na dosari zote zilizobainika zirekebishwe haraka na mradi ukabidhiwe tayari kwa matumizi yaliyokusudiwa ifikapo Disemba 30, 2023.
Ameagiza kazi zifanyike Usiku na mchana kwani Tayari Viongozi wa Chama na Serikali wamezuru mradi huo na kutoa maelekezo ya msingi kilichosalia ni utekelezaji wa maelekezo hayo na baada ya Disemba 30 hatua kali zitachukuliwa iwapo hakutakuwa na utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa