• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
Sikonge District Council
Sikonge District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Idadi ya Watu
      • Hali ya Hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Mifugo na uvuvi
      • Afya na Ustawi wa jamii
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mazingira na Taka ngumu
      • Kilimo, Umwagilaji na Ushirika
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Uchimbaji wa Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo Ndogo
    • Miongozo Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya sanaa
      • Sanaa za picha
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba
    • Habari mpya
    • Matukio

KAFUM YAIKAGUA KAMAGI

Imewekwa: May 10th, 2019

KAFUM YAIKAGUA KAMAGI

KAMATI ya Fedha, Uongozi na Mipango (KAFUM) ilitembelea shule ya Sekondari Kamagi ili kujionea namna mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa, bwalo la chakula pamoja na bweni la wanafunzi unavyoendelea.

Ikiwa shuleni hapo kamati hiyo ilifanikiwa kukutana na uongozi wa shule pamoja na  wanakamati wa ujenzi ambapo walielezea shuguli mbalimbali zinazohusu ujenzi,gharama na ununuzi wa vifaa  huku wakiitaja changamoto ya fedha kuonekana kutotosha kuukamilisha mradi huo.

Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango pamoja na walimu na wajunbe kamati ya Ujenzi wakizungumza na wanafunzi shule ya sekondari Kamagi walipotembele shuleni hapo.

Akijibu hoja hizo mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Peter Nzalalila ambaye pia ni mwenyeketi wa kamati ya Fedha, alitoa ushauri kwa wajumbe wa kamati ya ujenzi kuhakikisha wanawasimamia mafundi vizuri ili kazi ifanyike kwa uharaka na ubora unaotakiwa huku akikemea kisingizio cha pesa kutotosha. Akitolea mfano wa Wilaya ya Nzega ambayo imefanikiwa kumaliza mradi unaofanana na huo mapema  kwa fedha zilezile zilizotolewa kwenye mradi wa Kamagi hivyo kuitaka Sikonge ifuate nyayo hizo.

Miongoni mwa wajumbe waliochangia ni diwani wa kata ya Kipili Mhe. Maria Ngido aliyesema kuwa ni vyema pia ujenzi huo ukabana matumizi kwa kuongeza jengo la ofisi ya walimu kwa pesa  hizo zilizotolewa, huku akiitaja njia mojawapo ya kubana matumizi ni kushirikisha wananchi katika kujitolea kwani miradi hiyo imeletwa kwa ajili ya wananchi wa eneo hilo.

Akiongezea swala la kujitolea Mhe. Nzalalila alisema kuwa ni wakati sasa wa kutumia Skauti, Mgambo, pamoja Timu ya mpira wa mguu kujitolea katika ujenzi huo ambapo aliishauri kamati kuwapangia siku maalumu ya wao kushiri kwani uwepo wao katika jamii una mchango mkubwa ikiwemo kushiriki katika shuguli za maendeleo ikiwemo ujenzi unaoendelea Kamagi.

Shule ya sekondari Kamagi ilipata shilingi milioni 316,600,000 ikiwa ni fedha kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la chakula, vyumba vitatu vya madarasa, mabweni ya wanafunzi pamoja na matundu sita ya vyoo, hadi KAFUM inafika shuleni hapo ujenzi bado unaendelea ambapo mwenyekiti wa kamati ya ujenzi alisema kuwa wanatarajia kukamilisha baada ya siku 90 tokea fundi akabidhiwe mkataba wa ujenzi.

Mbali na kukagua miradi hiyo kamati pia ilishiriki kumwaga zege kwa kubeba kokoto ikiwa ni njia ya kuhamasisha wananchi wajitolee kwenye shughuli za maendeleo. Vile vile walizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kamagi ambapo walitoa ushauri kwa wanafunzi hao juu ya kuzingatia elimu wanayopewa kwa kuweka malengo katika masomo yao.

Mwenyekiti KAFUMU mwenye shati ya mistari Mhe. peter Nzalalila na wajumbe wakijitolea Kamagi Sekondari.


IMETOLEWA NA

KITENGO CHA TEKINOLOJIA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA)

SIKONGE.

Matangazo

  • TANGAZO LA ZABUNI YA KUKODISHA CANTEEN [MGAHAWA] MPYA KWENYE JENGO LA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZAABUNI YA KUMPATA MWEKEZAJI KATIKA KIWANDA CHA KATI CHA KUCHAKATA MAZAO YA NYUKI(MARUDIO) June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA USAFI KWENYE OFISI ZA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA ULINZI June 07, 2023
  • Angalia zaidi

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA MTEULE WA WILAYA YA SIKONGE MHE.THOMAS MYINGA ALA KIAPO KUANZA KAZI RASMI AKIRITHI MIKOBA YA MTANGULIZI WAKE MHE.CORNEL MAGEMBE

    July 02, 2025
  • WATUMISHI WA UMMA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIKONGE WAPIGWA MSASA JUU YA MATUMIZI YA MFUMO WA E-UTENDAJI (PEPMIS)

    June 25, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA SIKONGE YAPATA HATI INAYORIDHISHA TAARIFA YA UKAGUZI YA MWAKA 2023/2024

    June 14, 2025
  • UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA WAPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO KUTOKA 74% HADI 43% WILAYANI SIKONGE

    June 13, 2025
  • Angalia zaidi

Video

Ziara ya Waheshimiwa Madiwani Wilayani Rungwe - Mbeya.
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Matangazo
  • Zabuni
  • Matukio
  • Habari

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Mkoa wa Tabora
  • TAMISEMI
  • Urambo DC
  • UTUMISHI
  • Kaliua DC

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC

    Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora

    Simu: 0767135460

    Simu: 0767135460

    Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma zetu

Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa