KAFUM YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NYAHUA.
Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango(KAFUM) Wilayani Sikonge imetembelea Kata ya Nyahua na kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vitano,ofisi na matundu manne ya vyoo katika Shule ya msingi (Shikizi) ya Msonga na shule ya msingi Makibo.Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Rashidi Magope imejiridhisha na ujenzi wa vyumba vitatu na ofisi moja shule ya msingi Makibo iliyogharimu Tsh.Milioni 64.3 na kuwapongeza kwa juhudi zilizofanywa na kamati ya ujenzi kwa kumaliza katika ubora unaotakiwa sambamba na kuwahamasisha wananchi kuchangia kwa hiari.
Katika Shule Shikizi ya Msonga, taarifa ya ujenzi iliyosomwa na Mkuu wa Shule ya Msingi Nyahua stesheni ambae pia ni mlezi wa Shule shikizi ya Msonga amesema ujenzi wa madarasa mawili na ofisi moja umegharimu zaidi ya Tsh.milioni 29.1 ikiwa Milioni 25 ni kutoka Mpango wa lipa kwa matokeo (EP4R) na Tsh.Milioni 4 kutoka Mfuko wa jimbo pamoja na nguvu za wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji (W) Ndg.Selemani Pandawe amewapongeza Viongozi na wasimamizi wa ujenzi wa miradi hiyo licha ya changamoto wanazokumbana nazo huku akiwaasa kuendelea kusimamia vyema fedha za maendeleo zinazotolewa na Serikali.
Wananchi kata ya Nyahua wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kutoa fedha za miondombinu ya elimu na kuongeza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia wanafunzi kusoma katika mazingira bora.
Na.Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa