JEMBE LA UVCCM TAIFA KAZINI SIKONGE
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Ndugu. Kheri Denis James katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora, leo ametembelea Wilaya ya Sikonge na kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge na kuipokea taarifa ya ujenzi wa jengo hilo iliyosomwa na Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi, Mussa Mathias.
Mwenyekiti huyo wa UVCCM alipokuwa akitembelea jengo alimhoji Mhandisi anaejenga kama vijana wakazi wa Sikonge wamepata ajira katika mradi huo, baada ya kujulishwa kuwa vijana wamepata ajira alitoa faida ya kuwapa wakazi ajira katika miradi inayotekelezwa kuwa ni pamoja na kutohujumiwa kwa mradi na pia kupata kipato kwa vijana hao.
Aidha, Ndugu Kheri James amezungumza na wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wa chama na wajumbe wa kuu. "Heshima, ushirikiano baina yenu na bila kukwamishana katika majukumu yenu kutaleta maendeleo ya taifa letu" alisema ndugu Kheri James.
Alisisitiza kuwa Serikali kuu, Serikali za Mitaa na Chama wote ni kitu kimoja na tunatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi hivyo kutoelewana ni kukwamisha utekelezaji wa Ilani. “Wakubwa muwahurumie wadogo na wadogo muwaheshimu wakubwa” alisema ndugu Kheri na kuwaeleza tena kuwa heshima baina yenu ndo nguzo ya maendeleo ya taifa.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Peres Magiri alimshukuru sana Mwenyekiti huyo kwa hotuba nzuri yenye kujenga na isiyoisha hamu ya kuisikiliza na kusisitiza kuwa tuzingatie yaliyosemwa na kuyatekeleza ili kuleta maendeleo ya Taifa letu.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Sikonge, Edward Mwamotela kwa niaba ya Watumishi aliahidi kuwa watazingatia yote na kuimarisha mahusiano mazuri baina yao ili kuijenga Sikonge na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA TEHAMA SIKONGE
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa