IKOMBOLA CUP YAANZA RASMI.
Bonanza la michezo lijulikanalo kama Ikombola Cup laanza rasmi siku ya Jumapili ya Taarehe 30.6.2019 katika viwanja vya shule ya Msingi Misheni.
Bonanza hilo lililozinduliwa na mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Sikonge Renatus Mahimbali akiambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sikonge Mhe. Peter Nzalalila na Diwani wa kata ya Misheni Mhe. Juma Ikombola ambaye ndiye muandaaji wa mashindano hayo na mdhamini mkubwa.
Ufunguzi huo ulipambwa na michezo mbalimbali ikiwemo mashindano ya kunywa soda,kunywa soda na chapati, kuvuta kamba, mbio za magunia km. 100 kwa wanamme , na katika mbio hizi Jackob Erasto aliibuka kidedea baada ya kuwabwaga wenzake wakati kwa upande wa wanawake Mery Edward aliibuka mshindi.
Kwa upande wa mpira wa miguu timu ya Red star iliinyuka timu ya Usupilo mabao 6 kwa 0, ambapo dakika ya 24 kipindi cha kwanza mchezaji Albert Lukenzi aliindikia bao la kwanza timu ya Red star wakati bao la mwisho likifungwa dakika ya 88. Matokeo haya yanaiwezesha timu ya Red star kuingia hatua ya pili ya mpambano.
Bonanza hili limeandaliwa chini ya udhamini mkubwa wa Mhe. Juma Ikombola diwani wa kata ya Misheni, limefunguliwa leo hii na litafuatiwa na mwendelezo wa michezo mbalimbali ya mpira wa miguu na itashirikisha timu 8 kutoka kata Misheni. Na kilele cha michezo ni tarehe 7/7/2019
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa