Na, Edigar Nkilabo
Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete wameweka kambi katika hospitali ya wilaya ya Sikonge kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa na uchunguzi kwa wananchi wa wilaya ya Sikonge ikiwemo matibabu ya magonjwa ya moyo,mfumo wa mkojo,macho,pua pamoja na magonjwa ya ndani.
Akizungumza kutoka hospitalini hapo wakati zoezi la utoaji huduma za matibabu zikiendelea Mgaga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Sikonge Dkt.Catherine Katisho amesema serikali imewaletea karibu wananchi huduma za kibingwa ilimkuwapunguzia gharama za dkusafiri umbali mrefu kupata huduma hizo ambazo zitatolewa kwa muda wa siku tano.
“Hii ni fursa adhimu kwa wananchi wa Sikonge na vijiji vyake jitokezeni mje kupima mfanyiwe uchunguzi mpate matibabu ya kibingwa hapahapa hospitali ya wilaya, kwa huu muda wa siku tano kwa watu wa kata za mbali watapata muda wa kuja kupata huduma”amesema.
Kwa upande wake kiongozi wa msafara wa madaktari bingwa Dkt.Patrick Bilikundi amesema watatoa huduma za matibabu na uchunguzi wa magonjwa ya ndani, upasuaji na macho ikiwa ni mwendelezo wa nia njema ya serikali ya kuwasogezea huduma za kibingwa wananchi.
“Tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kuhakikisha wananchi wote wanaokuja hapa wanapata huduma bora na wale ambao watabainika kuwa na changamoto kubwa ya afya tutawapeleka hospitali ya rufaa ya mkoa Kitete ambapo watakutana na wataalamu wengine zaidi kwa ajili ya matibabu na watapata huduma kama ambavyo serikali imekusudia kusogeza huduma za afya karibu na wananchi”amesema.
Nao baadhi ya wakazi wa wilaya ya Sikonge waliojitokeza kupata huduma za kibingwa wamesema wamehudumiwa vizuri na wanaishukuru serikali kwa kuwasogezea karibu huduma ambazo hazipatikani mara kwa mara.
Kambi ya Madaktari Bingwa wilayani Sikonge inaendelea kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi hususani huduma za upasuaji, uchunguzi wa macho pamoja na matibabu ya magonjwa ya ndani kwa kipindi cha siku tano.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa