MVUA YALETA HASARA KUBWA .
Mvua kubwa iliyonyesha katika kata ya Kisanga kitongoji cha Ivunza wilayani Sikonge imefanya uharibifu mkubwa kwenye zao la tumbaku.
Mvua hiyo ya mawe ilinyesha siku ya jumamosi majira ya mchana ili inasadikiwa kuharibu zaidi ya Ekari 255 za Tumbaku zinazomilikiwa na jumla ya kaya 51 zote za wanakijiji wa Kisanga.
Akitembea kuagalia uharibifu uliotokea Mkuu wa Wilaya Sikonge Mhe. Peres Magiri aliwasisitiza wakulima kuwa na Bima ya kilimo ili kuwasaidia kupata fidia mara yanapotokea majanga kama hayo yaliyotokea. Hivyo basi alihimiza Kampuni ya Allience inayohusika na kilimo cha Tumbaku kufanya tathimini sahihi ya mazao yaliyoharibiwa na kujua thamani yake.
Mwnyekiti wa Halmashauri ya Sikonge akiangalia namna ambavyo uharibifu umefanyika.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sikonge Mhe. Peter Nzalalila pia alitembelea eneo hilo ili kujionea namna ambavyo wakulima wameathilika sanjari na kuzungumza na wakulima wenyewe. Mbali na kusisitiza kilimo chenye Bima pia alitoa pole kwa wote waliofikwa na janga hilo huku akikitaka chama cha msingi Kisanga kuangalia namna ambavyo wataweza kuwasaidia waathirika hao kufidia madeni yao ya pembe jeo waliyokopeshwa.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa Bi. Ambaye ni mkulima alisema kuwa kwa mwaka huu wa kilimo alikuwa amelima jumla ya Ekali 7 za tumbaku na alitegemea kuuza jumla ya kilo elfu 5 ndani ya chama chake cha msingi. Mwanamama huyo aliyeendesha kilimo hiko kwa nguvu zake mwenyewe wakati mume wake akiwa kitandani kwa ugonjwa, amepoteza mamilioni ya shilingi wakati akiendelea kubakiwa na mzigo mzito wa madeni ambayo anategemewa kukatwa mwaka unaofata wa kilimo endapo atalima tena.
Akilijibia swala hilo mwenyekiti wa chama cha msingi Kisanga alisema kuwa wao kama chama wataangalia namna ya kufanya kuwasaidia wakulima wote wzaliopata majanga ili wawe na moyo wa kurudi shambani awamu ijayo. Jambo ambalo lilipokelewa kwa mikono miwili na wakulima na pia kupongezwa na viongozi waliotembelea eneo hilo.
Naye diwani wa eneo hilo mh. Msumeno ambaye pia ni miongoni mwa wakulima waliopatwa na majanga hayo alitoa shukurani za dhati kwa wote waliotembelea kata yake na kusema kuwa wanafarijika kuona namna ambavyo serikali yao inawajali hata kipindi wanapopatwa na matatizo kama hayo.
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA TEKINOLOJIA HABARI NA MAWASILIANO
(TEHAMA)SIKONGE
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa