HALMASHAURI YACHANGIA ZAIDI YA TSH.MILIONI 647 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO SIKONGE.
Na.Anna Kapama.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Rashid Magope amesema kiasi cha Sh.milioni 647 zimetolewa na Halmashauri hiyo ikiwa ni sawa na asilima 76.42 ya lengo la kuchangia Zaidi ya Milioni 846 katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mh.Magope ametoa kauli hiyo wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Ndavukilo Wilayani hapo na kuongeza kuwa fedha hizo zimeelekezwa katika miradi mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa huduma za Afya,miundombinu ya madarasa katika shule za msingi na sekondari huku akiwasisitiza waheshimiwa Madiwani kuwahamasisha wananchi katika kata zao kujiunga na Mfuko wa bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa(iCHF) ili wananchi waweze kupata matibabu yaliyo bora na yenye gharama nafuu.
Aidha Mhe.Magope ametumia fursa hiyo kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa kuendelea kuwasimamia watumishi kwa usawa na ukaribu na kupelekea wananchi kupata huduma bora na stahiki huku akitoa rai kwa watumishi ambao bado wanafanya kazi kwa mazoea kuacha mara moja badala yake wachape kazi ili Halmshauri hiyo izidi kusonga mbele.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mhe.John Palingo amesisitiza suala la ukusanyaji mapato ikiwemo watendaji kuwasimamia vyema wakusanya mapato kwa kuwa fedha hizo ni muhimu katika kuendesha shughuli za maendeleo.
Nae Mkurugenzi Mtendaji(W) Selemani Pandawe amewasisitiza watumishi kushirikiana katika kutimiza adhima ya kutoa huduma bora na stahiki kwa jamii.
Katika Mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri ililenga kukusanya kiasi cha Sh.Bilioni 3.02 na kufikia mwezi Juni 2021 Halmashauri imefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh.Bilioni 2.4 sawa na asilimia 81.54 ya makusanyo yote ya lengo la mwaka mzima, fedha ambazo zitasaidia kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa