HALMASHAURI KUU CCM WILAYA YA SIKONGE YAAHIDI KUSIMAMIA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA SERIKALI.
Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Sikonge imefanya kikao na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi(2020-2025) ya Chama hicho kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Juni 2021.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo amesema hali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inaendelea.
"Kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Sikonge napenda kutoa pongezi za dhati kwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan...kwani Serikali hii imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja..tunajivunia ujenzi wa Barabara ya lami inayoendelea kujengwa kutoka Tabora kwenda Mpanda kupitia Sikonge, ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, ujenzi wa vituo vya Afya na Zahanati, ujenzi wa madarasa,matundu ya vyoo, na miradi ya Maji inayotekelezwa katika Wilaya yetu.Tunaahidi kushirikiana na Serikali kulinda Amani na usalama wa nchi sambamba na kufanya kazi kwa bidii" DC Palingo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sikonge Mhe.Anna Chambala amesema wataendelea kusimamia na kufatilia kila fedha inayotolewa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ili kuhakikisha ahadi walizoahidi zinatimia.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa