Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha leo ameshuhudia hafla fupi ya utiaji Saini wa Mkataba wa uendeshaji wa Kiwanda cha Kati cha Kuchakata na kufungasha mazao ya Nyuki katika Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Mhe. Chacha amepongeza kwa hatua iliyofikiwa leo kwani italeta tija kwa wanasikonge pamoja na nchi nzima kwa ujumla. “Tunashukuru lakini pia tunamatarajio makubwa kwamba tutapata manufaa zaidi kutokana na uwekezaji huu” amenena DC Chacha.
Akitambulisha wataalam pamoja na wageni waalikwa katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe amesema baada ya Mwekezaji kushinda zabuni hivyo anao wajibu wakukamilisha taratibu za kisheria ikiwepo kusaini mkataba wauendeshaji wa kiwanda kama ilivyofanyika leo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope akitoa salamu za Madiwani ameshukuru kufanyika kwa zoezi hilo la utiaji Saini kwani Kiwanda sasa kinakwenda kuleta faida nyingi kwa Wananchi wa Sikonge ikiwemo mapato kwa Halmashauri,Soko la uhakika kwa Wafugaji wa nyuki pamoja na ajira kwa vijana.
Aidha Ndg. Anthony Mwakipesile ambaye ndiye Mwekezaji wa Kiwanda hicho kupitia kampuni yake ya Ngonde Traders ameishukuru Serikali na Halmashauri kwa kupata nafasi ya kuwekeza katika kiwanda hicho ikizingatiwa kuwa watu wengi wamezoea kuona wawekezaji wasio wazawa ndio wanaopewa kipaumbele katika eneo la uwekezaji hivyo anaishukuru sana serikali kwa kuwajali wawekezaji wazawa wa nchi hii.
Zoezi hilo limeshuhudiwa pia na Wadau mbalimbali katika sekta ya biashara ya mazao ya nyuki,Benki ya CRDB pamoja na viongozi wa Chama na Serikali.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa