GARI LA WAZIRI LATUMIKA KUNASUA LORI.
Gari la Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph Kakunda latumika kunasua lori lililokuwa limekwama kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani Sikonge.
Katika Ziara hiyo Mhe. Kakunda pia aliambatana na mkuu wa wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Mgiri, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Peter Nzalalila pamoja na wataalamu kutoka Halmashauri ya Sikonge.
Waziri Kakunda alisimamisha msafara wakati akielekea katika kijiji cha Makibo kata ya Nyahua ili watoe msaada wa kulinasua lori lililokuwa limenasa kwenye tope kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Wilaya Sikonge kwa kutumia Gari lake. Alisema ‘’serikali ya awamu ya tano ipo kwa ajili ya wanachi wote hivyo basi hakuna kuendelea na msafara mpaka msaada utolewe na lori linasuliwe”
Gari la Mhe.waziri likivuta lori lililokwama katika mbuga ya Nyahua Wilayani Sikonge.
Dereva na watu waliokuwa ndani ya lori hilo walimpongeza Mhe. Kakunda kwa moyo huo na kustahajibu kwani walikuwa wanafikra kuwa waziri hawezi kushirikiana na wananchi wa hali ya chini, lakini kakunda ameshiriki kwa kutoa gari lake litumike kunasua lori huku yeye pia akishiriki kukata miti iliyoziba barabara na viongozi wengine akiwemo mkuu wa wilaya wakisukuma gari lililonasa.
Katika ziara yake ya siku tatu wilayani Sikonge Mhe. Waziri pia alikagua miradi mbali mbali ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari pamoja na barabara vilevile na uwekezaji wa kiwanda cha kuchata mazao ya alizeti kilichopo kata ya kiloleli kinachomilikiwa na bwana Sambarya ambacho kimekuwa kikitoa ajira zaidi ya 200. Ambapo ameagiza TIDO na SIDO kuja kiwandani hapo na kufanya utafiti ili waweze kuusaidia uwekezaji huo.
Pia alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi na kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi zinazowakwamisha kufikia uchumi wa Viwanda. Ambapo kwa kushirikiana na serikali ya wilaya ya Sikonge wamehaidi kuyashugulikia yale yote yaliyo ndani ya uwezo wao na mengine Mhe. Kakunda amehaidi kuyafikisha panapohusika huku akiendelea kusisitiza agizo la kufanya kazi kwa bidii.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa