VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUHUBIRI SHUGULI ZA KIUCHUMI.
Watumishi wa Mungu watakiwa kuwafundisha waumini wao umuhimu wa kufanya shuguli za kiuchumi zitakazowapatia kipato.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sikonge Bi. Martha Luleka alipoaliokwa kuwa mgeni rasmi na kupewa nafasi ya kufungua Mkutano wa Injiri ulioandaliwa na Umoja wa Makanisa Wilayani Sikonge unaofanyika katika Viwanja vya Tasaf wilayani humo.
Maombi mahalumu kwa Mkurugenzi wa Sikonge Martha Luleka aliyepiga magoti yakifanywa na wachungaji wa Umoja wa Makanisa
Bi Martha aliwataka watumishi hao wa Mungu kuwaongoza wahumini kujikita katika kufanya kazi halali kwani maendeleo hayawezi kumfata mtu anayeshinda muda wote kanisani akiomba bila kufanya kazi.
“waumini waakifanya kazi na kujipatia kipato halali watafanikisha shuguli za maendeleo ya kanisa na hata michango ndani ya kanisa watatoa kikamilifu sambamba na kuzisaidia familia zao” alisema
Sambamba na hayo pia aliwataka wananchi wa Sikonge kubadilika kitabia kupitia mkutano huo kwa kuacha kuvunja sheria za nchi na kujikita katika kushiriki kikamilifu katika shuguli za maendeleo pamoja na swala zima la usafi huku akisisitiza kuwasikiliza viongozi wao wa serikali na viongozi wao wa kidini.
Katika mkutano huo wachungaji walifanya maombi maalumu kwa Mkurugenzi Bi. Martha kwa utumishi wake uliotukuka sambamba na kuiombea serikali yaTanzania na viongozi wake ili wazidi kuiongoza nchi kwa amani.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa