DED SIKONGE AKAGUA HOSPITALI YA WILAYA.
Na.Anna Kapama
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Sikonge, Seleman Pandawe, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Sikonge ikiwa ni ziara yake ya kwanza baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Tito Luchagula ambae pia ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii.Pandawe amewapongeza wasimamizi wa ujenzi wa hospitali hiyo akiwemo Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya, Dkt.Theopister Elisa kwa usimamizi mzuri.Hospitali hiyo inayoendelea kujengwa imekamilika takribani majengo 10 na baadhi ya huduma za afya zimeanza kutolewa kwa upande wa wagonjwa wa nje (OPD).
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa