Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe ameongoza kikao cha kamati ya lishe kwa kipindi cha robo ya kwanza cha mwezi Julai hadi Septemba 2024, katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa viashiria mbalimbali vya lishe ngazi ya wilaya,Afisa lishe wilaya ya Sikonge Bi. Veronica Ferdinand amesema kwa asilimia kubwa viashiria vingi vimetekelezwa kwa ufanisi mzuri shabaha ikiwa ni kupambana na adui udumavu na ukondefu unaoathiri sana afya za wananchi hasa watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Aidha kwa upande wa changamoto zilizojitokeza katika kipindi cha robo hii ya kwanza ni pamoja na walezi/wazazi kushindwa kumaliza matibabu kwa kutoroka hospitalini pale wanapokuwa wameanzishiwa matibabu ya kupambana na utapiamlo mkali pamoja na mwitikio hafifu wa wazazi kuchagia chakula cha watoto shuleni.
Akifunga kikao hicho mweyekiti wa kamati ya lishe amatoa rai kwa wataalam kuongeza jitihada za kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kuchukua changamoto hizo kama chachu ya kuongeza ubunifu ili kuzitatua kwani ni changamoto zilizobainika ni za kawaida na zipo ndani ya uwezo wao.
“Twendeni tukasimamie na kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa hapa kwa ufanisi na haraka ,tukaondoe dosari zote zilizobainika katika robo hii ya kwanza.Sisi tupo tayari kuwasaidia pale mtakapohitaji msaada wetu.” Ameeleza Ndg. Pandawe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Ndg. Seleman Pandawe, ameahidi kuendelea kushirikiana na wataalam na wadau mbalimbali katika kuboresha utekelezaji wa mikakati ya lishe, ili kuhakikisha kuwa changamoto zinazojitokeza zinashughulikiwa kwa haraka na kwa ufanisi, na kwamba afya za wananchi, hasa watoto chini ya miaka mitano, zinaboreka kwa kiwango cha juu.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa