DED PANDAWE AKAGUA UJENZI WA MADARASA-UVIKO19.
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Sikonge Ndg.Selemani Pandawe amefanya ziara ya kushtukiza katika Shule za Msingi na Sekondari Wilayani hapo zilizopokea fedha za Mpango wa Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 ambazo zimetolewa na Serikali kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa shule za Sekondari na Msingi.
Aidha,DED Pandawe ametembelea Shule Shikizi ambazo zinaendelea na ujenzi wa madarasa ikiwemo Shule Shikizi ya Uyega, Mwakasembo, na Kiswahilini huku akiwasisitiza wasimamizi wa miradi kufanya kazi hiyo kwa uaminifu na kuwataka waepuke kuchelewesha miradi hiyo ambayo inatakiwa kumalizika ifikapo desemba 15,mwaka huu.
Aidha ,Ndg.Pandawe amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Uyenga Kata ya Igigwa kwa kusaidia ujenzi wa madarasa hayo huku akiwaasa wananchi maeneo mengine Wilayani hapo kujitolea kwa hiari kuchangia katika miradi ya maendeleo inayoletwa na Serikali kwa manufaa ya Wananchi.
Na.Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa