DC,DED MWENYEKITI WA HALMASHAURI NA WATAALAM SIKONGE WAFANYA ZIARA MANISPAA YA KAHAMA.
Na.Anna Kapama
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Seleman Pandawe , Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe.Rashid Magope na wataalam mbalimbali wamefanya ziara ya kikazi Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kwa lengo la kuona na kujifunza namna Manispaa ya Kahama inaendesha na kutekeleza Shughuli za Maendeleo ikiwemo uwekezaji na kuwawezesha wananchi kiuchumi .
Katika ziara hiyo ya Siku mbili Viongozi hao wamepata nafasi ya kutembelea Miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Manispaa hiyo ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Jengo la Ofisi za Manispaa , fursa za Kiuchumi, Uwekezaji , sambamba na kujifunza Mikakati na Mbinu za ukusanyaji wa Mapato ambavyo kwa pamoja Manispaa ya Kahama inafanya vizuri.
Ziara hiyo inatarajiwa kuleta tija katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa kuwa Rasilimali mbalimbali za kufanikisha zipo.
"Kwa ujuzi tulioupata hapa, tutaenda kuutumia kwa ajili ya kuiletea Maendeleo Wilaya yetu"DC Palingo.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe.Rashid Magope amesema kupitia ziara hiyo atakuwa Balozi kwa Waheshimiwa madiwani katika kuwaeleza Mikakati na Mbinu zilizotumiwa na Manispaa ya Kahama ili waweze kuzitumia kuwaletea wananchi Maendeleo
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg.Seleman Pandawe ameongeza kuwa kupitia ziara hiyo amejifujza Mikakati na Mbinu Bora za kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi na mengine mengi ambayo yakitekelezwa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge itapiga hatua za kinaendeleo .
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kahama Underson Msumba amesema njia moja wapo iliyowafikisha katika Maendeleo waliyonayo sasa ni kutumia fursa na Rasilimali zilizopo ikiwemo kuwawezesha wananchi kiuchumi na kupanga Mikakati madhubuti ya kuzitumia kwa manufaa ya wananchi pamoja Ushirikiano wa Viongozi na watendaji.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa