Sikonge_Tabora
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo ametembelea kaya za wanafatilia ambao wananufaika wa Mpango wa Serikali kunusuru kaya Masikini(TASAF) kutazama mwenendo wa maisha yao na jinsi wanavyotumia fedha hizo kuzalisha na kukuza kipato.
DC Palingo amewasisitiza wananchi kuzitumia fedha hizo kwa Uzalishaji ili kujiongezea kipato.
"Fedha hizi zina ukomo wake , lengo la Serikali ni kuwawezesha kujikwamua kiuchumi, mnapopata fedha hizi pamoja na mahitaji mengine nunua kuku, Mbuzi au hata Kodi Shamba ili Ulime ambapo shughuli zote hizi zitakuongezea kipato na kupiga hatua mbele kimaendeleo" amefafanua.
Kwa Upande wao badhi ya Wananchi wameishukuru Serikali ya awamu ya Sita kwa kuendelea kuwapatia fedha hizo kwani zimewanufaisha.
"Namshukuru Rais Samia kupitia fedha hizo nimenunua bati nikajenga nyumba nimenunua godoro na ninafuga Mbuzi na Kuku" Bi.Asha Rashid Mkazi wa Kiloli.
Namshukuru Mama Samia kupitia fedha za TASAF nimekodisha Shamba kwa ajili ya Kilimo, nimenunua mahitaji ya Wanafunzi ninaowalea hapa nyumbani Daftari na Sare za shule, kwa kweli sihangaiki Namshukuru sana" Mkazi wa Kijiji Cha Mwitikio, Mnufaika wa TASAF.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa