DC PALINGO AZINDUA MPANGO WA KUSAJILI NA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO WA UMRI CHINI YA MIAKA MITANO-SIKONGE.
Na.Anna Kapama.
3.6.2022
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo amezindua Mpango wa Kusajili na Kutoa Vyeti vya kuzaliwa kwa Watoto wenye Umri Chini ya Miaka Mitano Wilaya ya Sikonge na kuwataka Wananchi kutumia fursa hiyo kuwaleta watoto wasajiliwe na kupata vyeti vya kuzaliwa.
DC Palingo amesema mpango huo ni muhimu hivyo kila Mwananchi Mwenye mtoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano ana haki ya kusajiliwa na kupata Cheti Cha kuzaliwa Bure.
"Naishukuru Serikali kwa Kuleta Mpango huu katika eneo letu na pia naipongeza RITA kwa juhudi inazofanya katika kuleta mabadiliko chanya katika masuala ya Usajili" DC PALINGO.
Aidha, DC Palingo amewataka Wasajili Wasaidizi kutotumia mpango huo kama fursa ya kujipatia kipato .
"Natoa maelekezo kwamba yeyote atakaekiuka Misingi ya utendaji ya mpango huu kwa makusudi hatua zichukuliwe kwa mujibu wa Sheria" amefafanua.
Kwa Upande wake Mratibu wa Usajili wa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano Cloud Nkanwa amesema Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge inategemea Kusajili watoto 44,047 walio na Umri Chini ya Miaka Mitano na hawana vyeti vya kuzaliwa kwa muda wa wiki mbili na kuongeza kuwa mfumo huo utaendelea kuwepo ili kuweza kuwasajili na kuwapatia vyeti Watoto watakaozaliwa .
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa