Sikonge_Tabora
Na.Anna Kapama
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo amefanya Mkutano na Wananchi wa Kijiji Cha Kasandalala Kata ya Igigwa na kuzungumza nao maswala mbalimbali ikiwemo kuwasisitiza wananchi hao kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu sambamba na kutoa Ushirikiano pale matukio ya uvunjifu wa amani na Usalama yanapotokea yakiwemo mauaji ya raia.
"Kama tunataka tukomeshe matukio ya uhalifu Sikonge ni lazima wananchi tutoe taarifa za watu hao kama tunawajua ili waweze kutiwa hatiani na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria" DC PALINGO.
Aidha, amewasisitiza wananchi na Mgambo kutojichukulia sheria Mkononi wanapowakamata washukiwa wa uhalifu kwani kwa kufanya hivyo ni makosa kisheria badala yake wawapeleke kwenye mamlaka husika ambayo ni Kituo Cha Polisi .
"Watendaji, wahalifu wanapoletwa kwenu badala ya kuwapeleka Kituo Cha Polisi mnawapelekea Sungusungu, hilo ni kosa na kosa hilo lisijirudie tena" DC Palingo amesisitiza.
Kwa Upande wake Mkuu wa Polisi Wilaya ya Sikonge SSP.Zacharia Bura amewahakikishia usalama wa kutosha wananchi na kuwasihi kuendelea na shughuli zao za Uzalishaji huku akiwataka kutojihusisha na matukio ya uvunjifu wa amani na usalama, na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Sikonge linaendelea kuwashughulikia wote wanaoshukiwa kufanya matukio ya kihalifu.
Kwa Upande wao Vijana wa Kata hiyo wamemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo kuwapatia Mafunzo ya Mgambo ili kuweza kupata Elimu ya ulinzi na usalama Hatimaye kuimarisha ulinzi katika maeneo yao swala ambalo Mkuu wa Wilaya amewaahidi kulifanyia kazi na Mapema mwaka ujao Maafisa wa Jeshi la akiba watatoa mafunzo hayo.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa