Sikonge_Tabora.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo amepongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) katika Wilaya ya Sikonge Kwa kuendelea kusimamia zoezi la upandaji miti katika Wilaya hiyo tangu zoezi lilipozinduliwa mnamo Desemba 6, 2022.
DC Palingo ameyasema hayo Leo wakati akishiriki zoezi la upandaji miti katika Shule ya Sekondari Kamagi na kuwataka wananchi kuwa na utamaduni wa kupanda na kutunza miti ili kuhifadhi Mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi.
Awali akitoa taarifa ya mwenendo wa zoezi hilo Afisa wa TFS Linda Shio amesema TFS wameandaa Miche 50,000 Kwa ajili ya kupandwa na Kwa siku ya Jana Januari 24, 2023 jumla ya Miche 9846 ilipandwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo ikiwemo kata ya Tutuo na Kata ya Mkolye na mingine kugawiwa Kwa wananchi.
Aidha, DC Palingo amewashauri TFS kutoa Miche ya Matunda igawiwe Kwa wananchi mbali na kutunza Mazingira ikawe na Faida Kwa Chakula .
Zoezi la upandaji miti linaendelea na lengo la Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ni kupanda miti Millioni 1.5 Kwa Mwaka ikiwa ni kutii Agizo la Serikali la kupanda miti zaidi ya Millioni 1.5 Kwa Mwaka .
#kaziiendele
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa