DC PALINGO APONGEZA JUHUDI ZA WATAALAMU WA BONDE LA ZIWA TANGANYIKA KWA KUHIFADHI RASLIMALI ZA MAJI SIKONGE.
24.8.2022
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. John Palingo amewapongeza wataalamu wa Bodi ya Bonde la Ziwa Tanganyika kwa kuendeleza juhudi za kutunza na Kuhifadhi Raslimali za Maji ikiwa ni Pamoja na Bwawa la Utyatya huku akisisitiza Elimu itolewe kwa jamii ili chanzo Cha Maji Cha Bwawa la Utyatya kiweze kuendelea kutumika kwa wananchi wa Sikonge.
DC Palingo ameyasema hayo wakati akifungua mchakato wa kuunda Jumuiya ya Maji ya Bwawa la Utyatya sambamba na kuunda Bodi ya jumuiya watakaosimamia utunzwaji na utumiaji wa Raslimali za Maji kwa uwiano endelevu katika Bwawa la Utyatya mchakato uliosimamiwa na Bodi ya Bonde la Ziwa Tanganyika.
Awali Afisa Maendeleo ya jamanii Mwandamizi wa Bodi ya Bonde la Ziwa Tanganyika Bona Mremi amesema Bonde lilivutiwa na juhudi za jamii ya wafugaji sambamba na Halmashauri waliosimamia Ujenzi wa Mabirika ya kunyweshea Mifugo, sambamba na utunzaji wa Bwawa la Utyatya hali iliyopelekea Bodi hiyo kupanga Mikakati ya kuendeleza juhudi hizo ikiwemo kuunda jumuiya ya Maji.
Katika hatua nyingine Bonde la Ziwa Tanganyika limekabidhi Mizinga 20 kwa Jumuiya ya Maji, vifaa mbalimbali ili Jumuiya hiyo iweze kutekeleza majukumu yake ya utunzaji na usimamizi wa matumizi Bora ya Vyanzo vya Maji.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa