DC PALINGO AFANYA KAMPENI YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA.
Nyahua,
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. John Palingo ametembelea Kata ya Nyahua na kuzungumza na wananchi wa vijiji vya Nyahuanga,Nyahua stesheni na Makibo vinavyopatikana katika kata hiyo ikiwa ni ziara yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo, kuhamashisha ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na kusikiliza kero za wanachiDC Palingo amewasisitiza kujitolea kujenga vyumba vya madarasa ili Serikali kupitia mpango wake wa kujenga madarasa kwa tozo za miamala ziwakute wakiwa na maboma tayari,huku akiahidi kuchangia Sh.Laki moja kwa kila kijiji ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.Wakiwasilisha kero zao kwa Mkuu wa Wilaya,wananchi wa Kata hiyo wamesema kero kubwa ni pamoja na uchache wa Shule za msingi, upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayowapelekea wanafunzi kutembea umbali mrefu huku wakijaa kupita kiasi katika madarasa,huku kero nyingine ikiwa ni upatikanaji mgumu wa maji safi na salama na kukosekana kwa maeneo ya malisho ya mifugo.Aidha,DC Palingo ameagiza mradi wa ujenzi wa gati la maji unaoendelea umalizike haraka ili wananchi waweze kupata huduma ya maji,huku akiahidi kusimamia na kutatua kero zote zilizotolewa ikiwemo ya ujenzi wa madarasa.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nyahua Mhe.Andrea Masanja,amemshukuru Mhe.Palingo kwa kufanya ziara na kuzungumza na wananchi na kuahidi kusimamia utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa kwa maendeleo ya wananchi wa Nyahua.
Na.Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa