DC PALINGO AENDELEA NA ZIARA KITUNDA.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge ameendelea na ziara yake katika kata mbalimbali akikagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi.
Akikagua kituo cha Afya cha Mwitikio DC Palingo amewapongeza wahudumu wa Afya kwa kupunguza Idadi ya vifo vya mama na mtoto huku akiwaagiza viongozi wa Mfuko wa Bima ya Afya ya jamii iliyoboreshwa(iCHF) kuwaelimisha wananchi wa kijiji hicho ili wajiunge na Bima ya afya wapate huduma bora kwa gharama nafuu."Kupungunguza vifo vya mama na mtoto ni moja ya malengo ya kuwepo kwa vituo hivi"Mhe.Palingo aliongeza.
Katika mradi wa Maji Igumila ambao bado haujakamilika DC Palingo amewaagiza RUWASA kutekeleza kwa wakati ili wananchi Kata ya Kitunda wanufaike.
Akizungumza wananchi katika kijiji cha Mwitikio kata ya Kitunda, Mhe.Palingo amewataka watendaji kuwasomea wananchi taarifa ya mapato na matumizi pamoja taarifa za mienendo ya miradi inayotekelezwa ili wajue kinachoendelea katika vijiji vyao sambamba na kuwashirikisha katika kupanga miradi ya maendeleo.
Katika hatua nyingine DC Palingo ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea wananchi wa Sikonge miradi mingi ya Maendeleo ikiwemo vituo bora vya Afya, Elimu bila malipo, miundombinu ya barabara na Maji akiongeza kuwa Serikali ipo kuwahudumia wananchi.
Na.Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa