Na. Robert Magaka – Isongwa ,Sikonge – Tabora.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha ametembelea kijiji cha Isongwa kulichopo Kata ya Mkolye kuwapa pole na kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho waliokumbwa na maafa ya kukosa makazi ya kuishi baada ya nyumba zao kuanguka kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani Sikonge.
Katika ziara hiyo Mhe. Chacha ameambata na Katibu Tawala Wilaya ya Sikonge Ndg. Andrea Ngh’wani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe,Mkuu wa Divisheni ya Elimu Awali na Msingi Bi. Susana Makoye,Diwani Kata ya Mkolye Mhe. Omar Kategile pamoja na viongozi waandamizi wa kata hiyo.
Jumla ya nyumba 64 zimebomoka na kusababisha zaidi ya kaya 30 kukosa makazi ya kuishi katika kijiji hicho.Hata hivyo Mhe. Chacha ameahidi kuwapelekea misaada ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na Mahema ya kujisitiri na kuwatuma wataalam wa afya kutoa huduma za msingi za afya kwa waathirika wa maafa hayo.Kwa sasa wananchi hao waliokosa sehemu ya kuishi wanaishi kwa muda katika majengo ya Shule ya Msingi Isongwa.
Aidha Mhe. Chacha amewasihi kuzingatia maagizo ya Serikali hasa suala la uandikishaji wa watoto waliofikia umri wa kuanza shule kwani imebainika wananchi wa kijiji cha Isongwa kuwa na idadi ndogo kabisa ya uandikishaji mbali na kuwa Taarifa ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 inaonesha kijiji hicho kuwa na idadi kubwa ya watu kuliko vijiji vyote katika kata hiyo na wengi wa watu hao ni watoto wa umri wa kwenda shule pamoja vijana.
Mbali na maafa hayo kuwepo hakuna madhara ya vifo wala majeruhi yaliyojitokeza.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa