CMT YAAGIZA USHIRIKISHWAJI WA KAMATI ZA UJENZI ZA KATA/VIJIJI.
Na.Anna Kapama.
23.6.2022
Timu ya wataalamu (Wakuu wa Idara na Vitengo) imeagiza utekelezaji wa Miradi uzingatie Sheria na taratibu za Ujenzi wa Majengo ya Serikali huku ikiwaagiza Makatibu wa Miradi hiyo kuwashirikisha wajumbe wa Kamati za Ujenzi ambako miradi hiyo inatekelezwa katika katua zote za Ujenzi ikiwemo Manunuzi ma Mapokezi ya Vifaa vya Ujenzi kwa uwazi .
Hayo yamejiri leo wakati Kamati hiyo ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Seleman Pandawe ilipofanya ziara ya kukagua Jengo la Mama na Mtoto na Jengo la wagonjwa wa Nje(OPD) katika Kituo Cha Afya Nyahua , Jengo la kutolea huduma Kituo Cha Afya Tutuo , Ujenzi wa Shule ya Sekondari Nyahua, Madarasa matatu ya UVIKO-19 Shule ya Sekondari Kamagi na Kikundi Cha Vijana wajasiliamali ikiwa ni maandalizi ya kuupokea Mwenge wa Uhuru ifikako Mwezi Agosti,2022 .
#kaziiendelee
#jiandae kuhesabiwa
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa