CCM YAJITOSA KWENYE ELIMU.
WAZAZI wahimizwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni ili kubaini matatizo yanayowakabili watoto wao katika kufanya vizuri kwenye masomo.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Sikonge Bi. Anna Chambala alipokuwa kwenye sherehe za jumuhiya ya wazazi ya CCM ambapo kiwilaya ilifanyika Kata ya Chabutwa.
Katika sherehe hizo ambazo kwa mwaka huu zilibeba kauli mbiu iliyolenga kutoa elimu kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utafanyika kitaifa hapo mwishoni mwa mwaka 2019 ilisema kuwa “ Elimu, malezi na Maadili ni msingi wa uongozi bora hivyo mwaka huu wa 2019 tuchague viongozi bora na si bora viongozi”
Bi. Chambala alisema kuwa ni jukumu la wazazi wa CCM kusimamia maadili ya watoto ikiwemo Elimu na utendaji kazi kwani ni miongoni mwa misingi inayosimamiwa na Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha jamii inakuwa na vijana wenye maadili na weledi mzuri.
Aliongeza kuwa kitendo cha baadhi ya wazazi kutoshirikiana na walimu ili kuwabaini watoto watukutu kinapelekea watoto hao kujiingiza katika ajira mbaya. Alizitaja baadhi ya ajira hizo kuwa ni watoto kufanyishwa kazi za uyaya tofauti na umri wao, huku baadhi ya watoto wa kiume wakitumikishwa katika mashamba ya Tumbaku tena jambo hili likiungwa mkono na Wazazi husika huku jamii ikilifumbia macho. Ambapo alionya kuwa wao kama jumuiya ya wazazi ya CCM hawatalifumbia macho hata kidogo swala hilo.
Akionesha kuchoshwa na matokeo mabovu ya elimu WIlayani humo Mwenyekiti huyo alipiga marufuku kwa viongozi wote wanokaa maofisini tu bila kuingia katika jamii kufuatilia swala zima la elimu linavyoenda ili kujua namna wanavyoweza kusaidi kuinua kiwango cha Elimu Wilayani Sikonge. hivyo basi ni jukumu la kila mmoja moja kubadilika ili kutimiza wajibu wake utakaoleta matokeo chanya yenye maendeleo.
Mwenyekiti wa CCM Sikonge Bi. Anna Chambala akitoa msaada wa Sabuni kwa wazee wiki ya wazazi.
Viongozi mbalimbali Wilayani umo walipata wasaa wa kutoa maoni yao akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sikonge Mhe. Peter Nzalalila ambaye aliwahasa vijana kutumia fulsa ya barabara inyojengwa kutokea Tabora kuelekea Mpanga ikipitia Sikonge iwawezeshe kujikwamua kiuchumi na kuwa sehemu ya Kihistoria kuelekea mafanikio yao kwani wanaweza kuitumia kufanya biashara ndogondogo kama wafanyavyo vijana wa Chalinze Pwani.
Sherehe hizo pia ziliambatana na kupanda miti ikiwa ni miongoni mwa utunzaji Mazingira pamoja na kutoa misaada kwa wazee ambapo katoni mbili za sabuni zilitolewa kwa wazee kata ya Chabutwa ikiwa ni shukurani kwa ajili ya malezi yao mazuri yaliyopelekea kuwapata viongozi bora ambao wanatokea CCM.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa