Wazazi na walezi Wilayani Sikonge wametakiwa kuchangia chakula cha watoto shuleni na kuhakikisha watoto wanapata uji na chakula pindi wanapokuwa shuleni.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Tabora, Ndugu Said Nkumba alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi na kuzungumza na Wananchi wa tarafa ya Kiwere Wilayani Sikonge.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndugu Seleman Pandawe amesema watoto wakipata chakula shuleni hata ufaulu wao utaongezeka huku Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sikonge Bi.Anna Chambala akisema yeye amekuwa mstari wa mbele kuchangia chakula shuleni.
Aidha Mwenyekiti wa CCM mkoa amewataka walanguzi wa tumbaku kuacha mara moja kwani hatua Kali zitachukuliwa dhidi yao, kwakuwa adhima ya CCM ni kuhakikisha wakulima wananufaika na jasho lao kupitia kilimo.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Sikonge Mhe.Joseph Kakunda amesema ilani ya CCM Kwa Sikonge imetekelezwa Kwa asilimia 95 huku Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Rashid Magope akitoa shukrani za Wanasikonge kwa serikali.
Ziara hiyo ya siku mbili imehusisha ukaguzi wa miradi ya Elimu na maji pamoja na kusikiliza changamoto za Wananchi wa tarafa za Kiwere na Sikonge.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa