CCM KAZINI SIKONGE
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora, Majaliwa Bilali atembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Sikonge leo. Mradi huu ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dakt. John Pombe Magufuli katika Halmashauri 67 zilizopewa kila moja jumla ya Tsh. Bilioni 1.5 ambapo kila Halmashauri ilipewa muda hadi kufikia tarehe 30 Juni 2019 kukamilisha ujenzi huo.
Katibu huyo aliambatana na viongozi mbalmbali akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya, Bi. Anna Chambala, Katibu wa CCM Wilaya, Bwa. Emmanuel Mhene na Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Sikonge, Mhe. Peter Nzalalila pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Aidha, Katibu Mwenezi alipongeza juhudu zinazofanyika katika ujenzi huo na kuwataka viongozi wanaosimamia kukamilisha mradi huu kwa wakati ili wananchi wapate huduma iliyobora pamoja na changamoto zinazojitokeza katika kutekeleza mradi huu. Pia aliwataka viongozi wa Halmashauri kujenga uhusiano mzuri na viongozi wa CCM Wilaya ili kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015.
“Kama Injinia, wewe ndiye msimamizi wa shughuli zote za ujenzi zinazoendelea pale na Mganga Mkuu wa Wilaya ndiye mwenye Majengo yale, tujitahidi tunapotembelea mradi huu ili kupata taarifa tusiishie tu kwa wasimamizi wa majengo haya bali tusikilize na kero zinazowakuta vibarua wanaofanya kazi eneo hilo….” alisema Katibu huyo ili kutatua kero zinazosababisha ujenzi kususua kutokana na kutolipwa fedha zao kwa wakati. Hali hii imejitokeza katika eneo la mradi baada ya vibarua kuandamana na kutoa malalamiko yao kwa kiongozi huyo.
Naye Mhe. Peter Nzalalila, alishukuru kwa ujio wa Kiongozi huyo na kuahidi kusimamia maelekezo na maagizo hayo ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati pia aliwaomba viongozi wanaosimamia ujenzi kumpa taarifa yoyote yenye kupelekea ujenzi kususua au kukwama ili kwa pamoja washirikiane kuitatua. Baada ya hapo viongozi waliongozana kwenda katika kikao kingine cha Chama cha Mapinduzi (CCM).
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA TEHAMA SIKONGE @2019
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa