CANADA YAIFADHILI SIKONGE
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge yapokea ufadhili wa gari la kubebea wagongwa kutoka kwa watu wa Canada.
Akipokea Gari hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Sikonge Mhe. Peter Nzalalila alitoa shukurani zake kwa wahisani hao, na kuhahidi kuwa uwepo wa gari hilo litasaidia sana utoaji wa huduma za afya ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vya wamama wajawazito pamoja na watoto.
Aliongeza pia gari hilo liende kufanya kazi kwenye Zahanati ya Mibono ambako kuna uhitaji mkubwa hivyo uwepo wa gari hilo utachangia kuwahisha wagonjwa kwenye vituo vya Afya ili wapatiwe huduma zaidi.
Gari la kubebea wagonjwa lililotolewa kwa ufadhili wa watu wa Canada katika Halmashauri ya Sikonge.
Akikabidhi kwa niaba ya Mkurugugenzi Ndugu Yusuph Hamza alisema kuwa watazingatia maagizo yote yaliyotolewa na Mwenyekiti na kuhadi kulitumia gari hilo kwa madhumuni yaliyotolewa na wahisani wa Canada na si vinginevyo. Pia ali aliishukuru serikali ya jamuhuli ya muungano wa Tanzania kwa kuboresha sekta ya Afya hadi vijijini.
Akizungumza kwa niaba ya wataalamu mganga mkuu wa Wilaya Dkt Songoro alisema wamepokea kwa shukurani kubwa gari hilo na kuhaidi kulitunza vizuri ili liweze kutoa huduma kwa muda mrefu na kuokoa maisha ya watu.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa