Baraza hilo lililoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope limeridhia mapendekezo ya bajeti ya zaidi ya Tsh. Bilioni 40 kwa ajili ya Kwenda kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Akichangia hoja ya stahiki za waheshimiwa madiwani kutofautiana kati ya Manispaa ya Tabora na Sikonge Msimamizi wa Fedha Mkoa wa Tabora Bi. Shani Mangesho amesema posho na stahiki za waheshimiwa madiwani zipo kisheria na hazitofautiani kwani zinatokana na Muongozo uliopo na iwapo waheshimiwa watalipwa bila kuzingatia nyaraka na miongozo wanaweza kusababisha hoja kwa Mkaguzi wa Mkuu wa Hesabu za Serikali. “Mheshimiwa Mwenyekiti naomba niseme wazi kwamba Serikali yetu inaongozwa na waraka na miongozo.Na kama tutakwenda nje ya muongozo tunafanya kazi kinyume cha utaratibu na Mkaguzi ana haki ya kutuhoji kwanini hatukufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo.” Amesema Bi. Mangesho.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe wakati akichangia hoja katika baraza hilo amewashukuru wajumbe kwa michango yao mizuri na ameahidi ushauri wao utazingatiwa vema katika utekelezaji wa bajeti hiyo ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Akifunga baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope amewashukuru wajumbe kwa michango yao mizuri na yenye tija kwa Halmashauri hususani kwa kuridhia mapendekezo ya bajeti ambayo itakwenda kuwahudumia wananchi na kutatua chanagamoto mbalimbali za miundo mbinu na miradi mingine ya maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa