Baraza la wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge lililoketi leo limeridhia mapendekezo ya bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa mwaka wa fedha 2024/2025 baada ya kuijadili rasimu hiyo kwa kina na umakini mkubwa.
Akimwakilisha Mkuu wa Divisheni ya Mipango na uratibu Bi. Mkesika Mageta amesema Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imekadiria kutumia kiasi cha Shilingi 40,446,082,090 kwa mwaka ujao wa fedha katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo Wilayani Sikonge.
Baada ya wajumbe wa baraza hilo kujadili kwa kina rasimu hiyo walifikia uamuzi wa kuafiki kwa pamoja mapendekezo ya bajeti ambayo sasa itakwenda kutekelezwa kwa mwaka ujao wa fedha katika kuwaletea wananchi maendeleo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi Wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe alipokuwa akihitimisha mkutano huo amewashukuru wajumbe kwa Mawazo yao mazuri katika kuboresha vipengele mbalimbali vya rasimu hiyo na kutoa wito kwa wajumbe hao kuwa mabalozi wema kwa kufikisha ujumbe kwa watumishi wa umma juu ya mambo yote mazuri yaliyo kusudiwa katika utekelezaji wa bajeti hiyo kwa mwaka ujao wa fedha.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa