Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha aongoza baraza la Ushauri la Wilaya ya Sikonge kupitia bajeti inayopendekezwa kwa mwaka ujao wa fedha 2024/2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Aidan Frument Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu akiwasilisha rasimu ya bajeti hiyo amesema Halmashauri inakadiria kutumia kiasi cha Tsh. 40,446,082,090. Katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Wakichangia bajeti hiyo wajumbe wameshauri kuboreshwa kwa baadhi ya vipengele katika bajeti hiyo ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wake katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Sikonge.Wajumbe wametoa maoni hayo hasa katika eneo la Divisheni ya Mazingira,Maendeleo ya Jamii na Miundo mbinu.Wajumbe hao wameridhia kwa pamoja mapendekezo ya bajeti ya Halmashauri itakayokwenda kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Akifunga Kikao hicho Mhe. Chacha ameagiza Wataalam Kwenda kufanyia kazi mapendekezo yote ambayo wajumbe wameshauri katika kikao ili kuweza kufikia malengo ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Sikonge.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa