Sikonge_Tabora
Na.Anna Kapama
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge wamefanya ziara Mkoani Katavi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa ajili ya kujifunza usimamizi shirikishi wa Misitu na uuzaji wa hewa ya Ukaa ambayo ni chanzo kikubwa Cha Mapato katika Halmashauri hiyo.
Awali akiwakaribisha Madiwani na Wataalamu waliohudhuria Mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mhe.Hamad Mapengo amesema kupitia uuzaji wa hewa ya Ukaa Halmashauri imekusanya Mapato kufikia Tsh.Bilioni 4.2 katika Vijiji 8 vya Halmashauri hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 baada ya Kuhifadhi Misitu na kuzuia ukataji Miti katika maeneo yao.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. John Palingo amesema Wilaya hiyo inafanana kijiografia na Wilaya ya Tanganyika hasa katika Misitu hivyo mafunzo hayo yataleta tija katika kuanzisha mradi huo kwa kuwa tayari Misitu ipo .
"Tuna Hifadhi ya Misitu 5 inayomilikiwa na Halmashauri na Misitu 4 inamilikiwa na TFS ambapo ambapo Jumla tuna Misitu 9 hivyo naamini tukijifunza na kutekeleza tutaongeza Mapato katika Halmashauri yetu lakini pia kutunza Mazingira " DC Palingo.
Mkuu wa Kitengo Cha Maliasili na Uhifadhi Misitu Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bruno Nicholaus amesema Biashara ya Hewa ya Ukaa inahusisha wamiliki wa Viwanda Duniani ambavyo vinachangia kuchafua Mazingira hutoa fedha kwa maeneo yanayohifadhi na kutunza Misitu, Vyanzo vya Maji na Viumbe vilivyo hatarini kutoweka ili hewa chafu inayozalishwa na Viwanda hivyo iweze kufyonzwa na Misitu inayohifadhiwa ambapo Taasisi ya CARBON Tanzania inatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na Halmashauri.
#ZIARA INAENDELEA
#kaziendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa