Sikonge_Tabora
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge limepitisha makisio ya Mpango wa Bajeti Kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 ambapo TSH.Bilioni 29.4 ni Ruzuku ya Mishahara ya watumishi, Bilioni 3.67 ni Mapato ya Ndani, TSH.Bilioni 6.8 Miradi ya Maendeleo na , Millioni 729.4 Ruzuku ya matumizi ya kawaida.
Awali akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Rashid Magope amesema bajeti imepanda Kwa 30% ikilinganishwa na na Bajeti ya Mwaka WA Fedha 2022/2023 na kuongeza kuwa bajeti hiyo imejielekeza kutekeleza vipaumbele katika kuimarisha miundombinu ya Elimu, Afya, Kilimo,na Mifugo sambamba na kutoa Mikopo Kwa Vikundi vya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu vyenye mwelekeo wa Ujenzi wa Viwanda Vidogovidogo na ukamilishaji wa Jengo la Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri.
Kwa Upande wao baadhi ya madiwani waliopitisha bajeti hiyo wamesema itakuwa mkombozi katika kufanikisha utekelezaji wa mipango ya Maendeleo yaliyokusudiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge
"Bajeti ni nzuri ambayo Ndani yake imegusa sehemu nyingi katika Miradi ya Maendeleo ikiwemo kumalizia Miradi iliyoanzishwa Kwa Nguvu za wananchi, 10% ya Mapato ya Ndani itagawiwa Kwa Vikundi vilivyotajwa vya Wananchi hivyo ni bajeti ambayo inaenda kuleta neema kubwa Kwa wananchi wa Wilaya ya Sikonge" Mhe.Gasto Lwambano Diwani kata ya Kiloleli
"Bajeti ya Leo tuneipitisha Sisi madiwani kilichobaki ni utekelezaji tutashirikiana na wataalamu Kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo" Mhe. Josephine Aron Diwani kata ya Pangale.
Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya hutoa Mwongozo wa Makusudio na mtazamo wa Halmashauri katika kutekeleza majukumu yake ya Muda mfupi, Muda wa Kati na Muda mrefu , ugawaji wa Raslimali , Mapato na matumizi pamoja na usimamizi wa Mikakati na mipango katika kuleta Maendeleo Kwa Jamii.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa