ALAT YA CHANGIA UJENZI VYUMBA VYA MADARASA SIKONGE
Wajumbe wa ALAT mkoa wa Tabora wavutiwa na gharama ndogo zilizotumika katika mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Mbirani wilayani Sikonge.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa ALAT, Mhe. Adam Malunkwi walipokuwa katika ziara ya kukagua miradi mbalimbli ya maendeleo wilayani Sikonge siku ya tarehe 30 Novemba 2018, hivyo kuchangia kiasi cha milioni mbili (2000,000.00) ili kuunga mkono mradi huo. Mwenyekiti alizungumza kuwa pesa hizo zitumike kukamilisha angalau chumba kimoja cha darasa ili kianze kutumika.
akisoma taarifa fupi ya ujenzi mwalimu mkuu wa shule ya msingi mbirani. Ndg. Simoni Emmanuel alisema mradi huo wa ujenzi wa vyumba vinne (4) vya madarasa na ofisi moja (1) ya walimu umegharimu kiasi cha sh. 29,591,250 Mpaka sasa. Fedha ambazo zimepatikana katika mfuko wa jimbo, nguvu ya wananchi, programu ya lipa kwa matokeo (P4R) na mapato ya ndani ya Halmashauri.
HABARI PICHA:
Mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi katika shule ya msingi Mbirani.
Ndg. Emannuel aliongeza kuwa hadi kukamilika kwa mradi huo zinakisiwa kugharimu jumla ya shilingi 27,704,400.00. hii ikiwa ni jumla ya shilingi milioni 57,295,650.00 ambazo zilihitajika.
Katika ziara hiyo ambayo iliongozwa na mwenyekiti wa ALAT mkoa Alisema kuwa anatoa pongezi za pekee kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa jitihada zao kwenye sekta ya elimu. Pia kwa kubana matumizi ambapo wameweza kujenda boma la vyumba vinne vya madarasa na ofisi moja ya walimu kwa gharama ndogo.
Wakiambatana na wenyeji wao wakiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bi. Martha Luleka pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mhe. Peter nzalalila walizipokea shukurani hizo na kuahidi kutumia pesa zilizotolewa ili kukamilisha ujenzi wa chumba kimojawapo cha darasa jambo litakalo saidia kupunguza msongamano wa wanafunzi.
Wajumbe wa ALAT walitoa msisitizo kwa Halmashauri zingine juu ya kuwa na nidhaamu katika fedha na kuitolea mfano Halmashauri ya Sikonge kupitia mradi huo, kwani kwa kufanya hivyo kunaunga jitihada za Mhe. Raisi Dkt John Pombe Magufuli katika kubana matumizi na kipaumbele chake katika sekta ya elimu.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa