UJIO WA MADAKTARI BINGWA SIKONGE
Mkuu wa wilaya, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya na mkurugenzi mtendaji wa wilaya, wanayofuraha kuwatangazia wananchi wa wilaya ya sikonge, kwamba kutakuwa na ugeni wa madaktari bingwa ambao watafanya uchunguzi na tiba kwa wananchi wa sikonge na wilaya jirani kuanzia tarehe 26 februari 2018 hadi 2 machi 2018. Jopo hilo la Madaktari zaidi ya 30 wapo katika kundi lijulikanalo kama "JITOLEE GROUP" na wanafani mbalimbali. Kuna mabingwa wa upasuaji, Bingwa wa kinamama, Bingwa wa pua,koo na masikio, Bingwa wa ngozi, Bingwa wa macho na meno. Hivyo, kama huduma ulikuwa uifuate Mhimbili au Bugando na kwa kutumia gharama kubwa, sasa huduma imekufuata karibu kabisa. Huduma zitakuwa katika sehemu mbili (Vituo viwili), katika kituo cha Afya Mazinge na Hospitali teule ya Wilaya CDH. Mnakaribishwa sana.
WENYE BIMA ZA AFYA, KADI ZAO ZITATUMIKA NA KWA WANANCHI AMBAO HAWANA BIMA SERIKALI ITAGHARAMIA.
Karibuni sana
Imeandaliwa na Kitengo cha TEHAMA Sikonge
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa