• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
Sikonge District Council
Sikonge District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Idadi ya Watu
      • Hali ya Hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Mifugo na uvuvi
      • Afya na Ustawi wa jamii
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mazingira na Taka ngumu
      • Kilimo, Umwagilaji na Ushirika
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Uchimbaji wa Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo Ndogo
    • Miongozo Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya sanaa
      • Sanaa za picha
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba
    • Habari mpya
    • Matukio

HATI YENYE MASHAKA

Imewekwa: August 16th, 2019

SIKONGE WAPEWA WIKI MBILI  KUJIBU HOJA ZOTE ZA CAG ZILIZOSABABISHA WAPATE HATI YENYE MASHAKA

NA EVELINA ODEMBA.

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeiagiza Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kuhakikisha ndani ya wiki mbili imemaliza kujibu hoja 68 za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zilizosalia  ili ziweze kufutwa kwa kutoa vielelezo vinavyohitajika.

Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani cha kupitia hoja ya mbalimbali  za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018.

Alisema hoja hizo ndio zimesababisha Halmashauri hiyo kuwa kati ya Halmashauri saba nchini zilizopata Hati yenye shaka, ni lazima zijibiwe kwa kuwasilisha vielelezo vitakavyothibitisha matumizi ya fedha hizo kama yalifuata taratibu.

Mwanri aliwataka Wakuu wa Idara na Vitengo vya Halmashauri hiyo kuhakikisha wanatumia wiki hizo kutoa vielelezo ambavyo vitamwezesha Mkaguzi kufuta hoja.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa alimwagiza Katibu Tawala Mkoa wa Tabora kuhakikisha waliokuwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ambao wamehamia Halmashauri nyingine na ambao wametajwa kwenye hoja za CAG warudishwe ili waje kujibu hoja.

Watumishi hao ni pamoja na aliyekuwa Mganga wa Wilaya (DMO), Afisa Utumishi (DHRO) na Mweka Hazina wa Wilaya(DT).

Alisema kwa kuwa watumishi hao wametajwa katika taarifa ni vema warudi ili waje kujibu hoja zao na kurudisha fedha ambazo zimeonyeshwa kwenye vitabu vya CAG.

Akisoma taarifa kwa niaba ya Mkaguzi Mkuu wa Nje, Christopher Chalo alizitaja sababu zilizopelekea kupata Hati yenye shaka kuwa ni pamoja na kutokuhakikiwa kwa vitabu 27 vya kukusanyia mapato, kuwepo kwa viashiria vya ubadhilifu katika matumizi ya fedha mbalimbali zenye thamani milioni 128,matumizi ya fedha za mapato ya ndani kabla ya kupelekwa Benki shilingi milioni 55.8.

Sababu nyingine ni fedha za EGPAF zilizotumika katika shughuli zisizojulikana kiasi cha milioni 73.2, fedha za posho zilizochukuliwa benki na kulipwa bila wahusika kukiri mapokezi milioni 29.3,kukosekana kwa hati za malipo za kiasi cha milioni 18.1.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sikonge Mhe. Peter nzalalila akisoma dua maalum wakati wa baraza. pembeni ni Mkurugenzi wa Halmashauri Martha Luleka

Alisema sababu nyingine ni malipo yenye nyaraka pungufu kiasi cha milioni 15 na makusanyo ya papo kwa papo ambayo hayakupelekwa benki kiasi cha milioni 5.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema watawachukulia hatua watumishi wote ambao wameisababishia Halmashauri hiyo kuzalisha hoja za kiukaguzi za kiukaguzi na kupata Hati yenye shaka.

Alisema watumishi ni vema wakajitahidi kuzuia hoja na sio kutoa maamuzi ambayo yanasababisha kuendelea kuzalisha hoja kila mwaka .

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora aliitaka Menejimenti ya Halmashauri hiyo kuunda timu ya kushughulikia hoja hizo ili ndani ya Mwezi mmoja wawe wamejibu na kufuta hoja hizo.

Makungu aliwaomba Madiwani kuhakikisha wanafuatilia katika Kata zao ili miradi mbalimbali ya wananchi iwe na ubora unaotakiwa.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Peter Nzalalila alisema wameunda timu ya Madiwani na Wataalamu watakaochunguza watendaji waliosababisha wapate Hati yenye shaka ili waweze kuchukuliwa hatua.

Mwisho

Matangazo

  • TANGAZO LA ZABUNI YA KUKODISHA CANTEEN [MGAHAWA] MPYA KWENYE JENGO LA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZAABUNI YA KUMPATA MWEKEZAJI KATIKA KIWANDA CHA KATI CHA KUCHAKATA MAZAO YA NYUKI(MARUDIO) June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA USAFI KWENYE OFISI ZA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA ULINZI June 07, 2023
  • Angalia zaidi

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA MTEULE WA WILAYA YA SIKONGE MHE.THOMAS MYINGA ALA KIAPO KUANZA KAZI RASMI AKIRITHI MIKOBA YA MTANGULIZI WAKE MHE.CORNEL MAGEMBE

    July 02, 2025
  • WATUMISHI WA UMMA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIKONGE WAPIGWA MSASA JUU YA MATUMIZI YA MFUMO WA E-UTENDAJI (PEPMIS)

    June 25, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA SIKONGE YAPATA HATI INAYORIDHISHA TAARIFA YA UKAGUZI YA MWAKA 2023/2024

    June 14, 2025
  • UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA WAPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO KUTOKA 74% HADI 43% WILAYANI SIKONGE

    June 13, 2025
  • Angalia zaidi

Video

Ziara ya Waheshimiwa Madiwani Wilayani Rungwe - Mbeya.
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Matangazo
  • Zabuni
  • Matukio
  • Habari

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Mkoa wa Tabora
  • TAMISEMI
  • Urambo DC
  • UTUMISHI
  • Kaliua DC

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC

    Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora

    Simu: 0767135460

    Simu: 0767135460

    Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma zetu

Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa